TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA KUJITOLEA KWA WAWEZESHAJI NGAZI YA JAMII
Wizara ya maji kupitia Bodi ya Maji Bonde la Rufiji inatekeleza Mradi wa kuimalisha mbinu za asili za usimamizi wa vyanzo vya maji na kukabiliana na mabadiliko ya Tabia inchi katika Bonde la Usangu. Mradi huu unafadhililiwa na serikali ya Japani kuputia Benki ya Dunia. Mradi wa unatekelezwa katika Vijiji 45 katika Wilaya ya Mbarali katika kata za Madibira,Kongoro,Igava, Chimala, Mapogolo, Mahongole,Ubaruku,Itamboleo,Mwatenga,Luhanga,Lugelele,Mawindi na Ihai, Mkoa wa Mbeya.
Mradi utasaidia uanzishaji wa Vikundi vya Uhifadhi vya kijamii (Community Consevartion Banks-COCOBA). Ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli ya uundaji wa vikundi,Mradi utashirikisha wawezeshaji ngazi ya jamii ambao watasaidia shughuli za uendeshaji wa vikundi wakati wa awali wa uanzishaji wa Vikundi. Bodi inatangaza nafasi za kazi za kujitolea kwa wawezeshaji ngazi ya jamii.
SIFA ZA MUUOMBAJI
- Awe ni mwananchi Mkaazi wa Kata au vijiji husika.
- Awe na umri usiozidi miaka 30.
- Awe na elimu ya Sekondari.
- Awe na elimu ngazi ya cheti kutoka chuo cha Maendeleo ya jamii, Maendeleo Vijijini, Ustawi wa Jamii au Afya ya Jamii.
- Waombaji wa jinsi ya kike wanahamasishwa kuomba.
- Maombi ya yaipitishwe na Mtendaji wa Kijiji au kata husika.
MAWASILIANO
Maombi yapelekwe kwa mkono Kwenye Ofisi za Maji Bonde la Rufiji -Rujewa, Mbarali.
Mwisho wa Maombi ni tarehe 15/11/2025 saa 12 Jioni. Kwa masiliano piga 0685 561 948 au
0713 502 096
LIMETOLEWA NA MKURUGENZI
BODI YA MAJI BONDE LA RUFIJI
MAKAO MAKUU-IRINGA

