Kibali cha Uchimbaji wa Visima

Bodi ya Maji Bonde la Rufiji inatoa huduma ya kutoa kibali cha uchimbaji wa visima kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Namba 11 ya mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2022
Huduma hii inapatikana kwa kufuata taratibu zilizopangwa kwa kujaza fomu ya Maombi ya kibali cha uchimbaji wa visima na kuiwasilisha katika Ofisi ya Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji kupitia anuani iliyopo kwenye fomu hiyo. Bonyeza hapa ili kupakua fomu ya maombi ya kibali cha uchimbaji wa Kisima.
Pia kupitia mfumo wa WUMIs, Mteja anaweza kujaza fomu na kuiwasilisha mojakwamoja kupitia mfumo huo. Bonyeza hapa ili kufanya maombi ya Kibali cha uchimbaji wa Kisima.