Mpango kazi wa Bonde la Rufiji kwa mwaka 2020/21 hadi 2024/25 unaelezea hatua na matokeo yanayopaswa kufikiwa na jinsi utendaji utavyopimwa. Mpango huu unabainisha masuala na mikakati ya kushughulikia matatizo magumu hasahasa yanayohusiana na Rasilimali za Maji ndani ya Bonde. Mpango kazi wa Usimamizi wa Rasilimali za Maji unakusudia kuongoza Bonde katika kutatua changamoto zake za usimamizi wa Rasilimali za Maji, na Mpango unapendekeza mfululizo wa mikakati, malengo na kutambua kitengo/sehemu ya kuitekeleza. Wafanyakazi wa Bonde la Rufiji na wataalamu wa nje wamefanya kazi kubaini Maono, Dhamira, Thamani za Msingi, Masuala Muhimu, malengo ya kimkakati matano (5) na shughuli 28 zinazohusiana na Bonde hilo kwa kipindi cha miaka mitano.
Bonyeza hapa kufungua Mpango kazi wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji