UJENZI WA BIRIKA MABADAGA KUKAMILIKA.
Imewekwa: 10 Oct, 2024
UJENZI WA BIRIKA MABADAGA KUKAMILIKA.

Ujenzi wa birika za kunyweshea mifugo katika vijiji vitano (5) wilaya ya Mbarali unaotekelezwa na Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kupitia mradi wa kukuza na kuendeleza utalii kusini REGROW umefikia hatua nzuri baada ya birika la kijiji cha Mabadaga pamoja na kisima cha kusambaza maji katika birika hilo kuwa limekamilika.
Kwa ujumla kazi ya ujenzi wa birika zote tano (5) ipo ukingoni na inatarajiwa kutatua changamoto ya uharibifu wa kingo za mito hivyo kupunguza upotevu wa Maji mtoni. Kila tone lina Thamani