JUKWAA LA WADAU KUHUSU UTEKELEZAJI WA MRADI WA REGROW
Imewekwa: 10 Oct, 2024
JUKWAA LA WADAU KUHUSU UTEKELEZAJI WA MRADI WA REGROW

Jukwaa la Wadau wa usimamizi wa Rasilimali Maji lenye lengo la kujadili utekelezaji wa shughuli za mradi wa REGROW unaotekelezwa na Bodi ya Maji Bonde la Rufiji katika kidakio cha Great Ruaha limefanyika leo tarehe 04/04/2024 katika ofisi ndogo ya Bonde la Rufiji kidakio cha Great Ruaha-Rujewa Mbarali.
Jukwaa hilo limehusisha wadau mbalimbali kutoka sekta tofauti ambao wametoa michango yao juu ya shughuli zinazotekelezwa na mradi wa REGROW wenye lengo la kuboresha usimamizi wa Rasilimali za Maji ili kuongeza mtiririko wa Maji katika Mto Ruaha Mkuu na kuimarisha shughuli za utalii.