Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kuhesabu watumia maji na vyanzo vya maji.
08 Oct, 2024 Pakua

 

Bodi ya Maji Bonde la Rufiji ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya maji yenye jukumu la kusimamia rasilimali za maji. Kazi ya usimamizi wa rasilimali za maji ni pamoja na kufanya tathmini ya rasilimali za maji, kugawa maji,  kutunza vyanzo vya maji na kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji.  

 

Katika kutekeleza majukumu yake, Bodi inakutana na changamoto mbalimbali ikiwemo utekelezaji duni wa sheria kuhusu matumizi ya maji kutoka katika vyanzo. Watumiaji wengi hutumia maji kinyume na sheria (bila vibali) hali ambayo inasababisha Bodi kutokuwa na taarifa/takwimu sahihi ya hali ya maji.

 

Bodi ya Maji Bonde la Rufiji imepanga kufanya tathmini ya watumia maji wote kwa lengo la kujua wenye vibali ni wangapi na wasio na vibali ni wangapi, hii itasaidia kuweka mizania katika hali ya usahihi. Pia Bodi itatambua vyanzo vya maji vinavyotumika na vitakavyotumika na miji mbalimbali na kuvitunza. Zoezi hili litafanyika kwa muda wa miezi miwili kutoka sasa.

 

Hivyo, Bodi ya Maji Bonde la Rufiji inaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi, kwa kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia utunzaji wa rasilimali za maji.